logo

VIJANA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA UKATILI -JOYCE NYANGI

Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Morogoro Shujaa Bi. Joyce Hamis Nyangi amewaasa vijana wahitimu wa CASFETA na UKWATA kujiepusha na vitendo vya ukatili vinavyofanyika kwenye jamii zetu.

‎.

‎Bi. Joyce ameyasema hayo Novemba 06,2025 alipokuwa ameshiriki mahafali ya kidini ya CASFETA na UKWATA katika Chuo Cha FDC kilichopo Ilonga.

‎.

‎Mwenyekiti huyo alitoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa kuelezea maana na aina ya ukatili,jinsi ya kuripoti na kuepuka vitendo vya ukatili.

‎.

‎Aidha, Amewaasa vijana kuilinda amani tuliyonayo na kutoa taarifa kwa vyombo husika endapo wataona viashiria vya kuvunjika kwa amani vipo.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn