QUEEN LUGEMBE AJAZA MAMIA KWENYE UZINDUZI WA KAMPENI ZA UBUNGE JIMBO LA UBUNGO
Wananchi wa Ubungo pamoja na wafuasi wa Chama cha ACT Wazalendo wamejitokeza kwa wingi leo katika viwanja vya Manzese Bakhresa, kushuhudia uzinduzi wa kampeni za ubunge wa mgombea wa Jimbo la Ubungo, Bi. Queen Julieth Lugembe.
Uzinduzi huo umempa nafasi Bi. Queen Julieth kuzungumza moja kwa moja na wananchi wa jimbo hilo, akieleza ahadi zake na mipango yake ya maendeleo endapo atapata nafasi ya kuliongoza Jimbo la Ubungo baada ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.
Aidha, Wanachama wa ACT Wazalendo na wakazi wa Ubungo wameonyesha mshikamano na hamasa kubwa, wakisisitiza umuhimu wa kuleta mabadiliko na maendeleo kupitia sera na dhamira ya mgombea wao.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

