
DAWATI LA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA LATOA ELIMU YA KISHERIA KWA WANANCHI WA KATA YA IRINGA MVUMI MKOANI DODOMA
Kuelekea Maadhimisho ya Jukwaa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mwaka 2025 yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Dodoma, Dawati la Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Limeshiriki kutoa elimu ya kisheria kwa wananchi wa kata ya Iringa Mvumi wilaya ya Chamwino.
Katika zoezi hilo, migogoro mingi iliyobainika ni migogoro ya ndoa, hali iliyopelekea kutoa elimu na baadhi ya kesi hizo kuchukuliwa kwa ajili ya kufanyiwa kazi katika hatua za juu zaidi.
Aidha, baadhi ya wananchi wamelishukuru Dawati hilo kwa kuwa limesaidia katika kutoa Elimu na kuwapa uelewa juu ya mambo mbalimbali ya kijamii ambayo hapo awali walidhani ni masuala ya kisheria
Maadhimisho ya Jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali mwaka 2025 yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 13 Mwezi Agosti katika ukumbi wa Jakaya Kikwete.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news