logo

MADAKTARI BINGWA WA BMH ‎WAHUDUMIA WAGONJWA 2897 NCHINI BURUNDI

Mke wa Rais wa Burundi Bi. Angeline Ndayishimiye leo Julai 31,2025 amehitimisha kambi ya Madaktari bingwa wa Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyokuwa ikifanyika nchini humo.

‎.

‎Akiwa anahitimisha kambi hiyo, Bi. Angeline amesema bado Madaktari Bingwa wanahitajika nchini Burundi kutoa huduma ya matibabu kwa jamii.

‎"Niwapongeze Madaktari wa Hospitali ya Benjamin Mkapa mmetusaidia sana kuhakikisha ndugu zetu wanapata matibabu na wanapona,bado uhitaji ni mkubwa sana hivyo tunatarajia mtarejea muda si mrefu" alisema Mhe. Angeline.

‎Kwa upande wa Balozi wa Tanzania nchini Burundi Galasius Byakanwa amesema kuwepo kwa kambi hii ni tafsiri tosha ya kuwafuta machozi, kuongeza furaha na kuokoa maisha ya wagonjwa wa Burundi.

‎"Wagonjwa walioonwa na madaktari wetu ni 2897, katika hawa waliofanyiwa upasuaji ni 211 katika wiki hizi tatu na wote wanaendelea vizuri.

‎.

‎"Katika kambi hii kuna watoto 32 wanahitajika kupewa matibabu zaidi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, watoto hawa wana shida ya moyo, hata hivyo ubalozi wa Tanzania nchini Burundi utawasomesha Madaktari wawili walioonesha juhudi ya kujifunza mmoja ni kutoka Hospitali ya Gitega na mwingine ni wa hapa" alisema Balozi Byakanwa.

‎Hospitali ya Benjamin Mkapa imeendelea kufanya utalii wa matibabu katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na kati, lengo ikiwa ni kutoa huduma hizo kwa wananchi wa maeneo hayo.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn