GEITA KUONDOKANA NA MATUMIZI YA ZEBAKI NCHINI IFIKAPO MWAKA 2030
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Martine Shigela, amesema Mkoa huo kupitia Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan umesaini mikataba yenye lengo la kuwaondoa wachimbaji wadogo katika matumizi ya Zebaki katika zoezi la Uchenjuaji wa madini ya aina ya Dhahabu.
.
Shigela ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Watanzania kupitia mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita yaliyopatikana katika mkoa huo leo Julai 21, 2025 katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dodoma.
.
Amesema mpaka hivi sasa kuna ongezeko la mitambo 13 ya kisasa inazotumiwa kuchenjua dhahabu hivyo kukamilisha mitambo 23.
.
Aidha, Shigela amesema wameweka jitihada ili ifikapo 2030 waweze kuondoka kwenye matumizi ya Zebaki na kuingia kwenye matumizi ya kisasa, kwani ni hatari kwa Afya ya binadamu na mazingira kwa ujumla.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

