logo

PATO LA MKOA WA TANGA ‎LAONGEZEKA KUTOKA TRILIONI 6.818 HADI TRILIONI 9.581 MWAKA 2024

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian amesema kwa mujibu wa Takwimu za NBS kwa mwaka 2024, pato la Mkoa huo (GDP) limeongezeka kutoka wastani wa shilingi Trilioni 6.818 kwa mwaka 2020 hadi shilingi Trilioni 9.581 kwa mwaka 2024 sawa na asilimia 4.7 ya Pato la Taifa ambalo ni shilingi Trilioni 205.846.

‎.

‎"Takwimu hizi zinauweka Mkoa wa Tanga kushika nafasi ya sita (6) kati ya Mikoa yote ya Tanzania Bara katika vita dhidi ya umaskini pamoja na mchango wa pato la Taifa" alisema.

‎.

‎Balozi Dkt. Burian ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Watanzania kupitia mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika mkoa huo leo Julai 15,2025 katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dodoma.

‎.

‎Amesema wastani wa pato la Mtu mmoja (Per Capital Income) limeongezeka kutoka wastani wa shilingi milioni 2.783,908.00 kwa mwaka 2020 hadi shilingi milioni 3,433,368.00 kwa mwaka 2024.

‎.

‎Kwa upande mwingine, Balozi Dkt. Burian amesema Mkoa wa Tanga una jumla ya vijiji 763 ambapo vijiji vyote sawa na asilimia 100 vimepata huduma ya umeme kupitia miradi ya awali kama vile REA awamu ya kwanza (REA I), REA awamu ya pili (REA II), REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza (REA III Round I), na REA awamu ya tatu mzunguko wa pili (REA III Round II).

‎ .

‎"Jumla ya Vitongoji 2,382 vimefikiwa na huduma ya umeme kati ya vitongoji 4,531 vya mkoa wa Tanga ikiwa ni sawa na asilimia 52.6 ya vitongoji vyote.

‎.

‎"REA wamepanga kufikisha umeme katika vitongoji 180 kupitia mradi wa HEP 2A ambapo Mkandarasi amepatikana mwezi April, 2025 na pia vitongoji 673 viko katika mpango wa kufikishiwa umeme kupitia mradi wa vitongoji HEP 2B unaotegemewa kuanza utekelezaji wake katika kipindi cha mwaka wa fedha 2025/2026" alisema Balozi Burian.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn