logo

WAZIRI NAPE AMESEMA BILIONI 212.457 BAJETI YA WIZARA YA HABARI

WIZARA ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi Bilioni 212.457 Katika Mwaka wa Fedha 2023/24.

Ombi hilo limewasilishwa Bungeni na Waziri wa wizara hiyo Mhe.Nape Nnauye na kufafanua kuwa Kiasi cha zaidi Shilingi Bilioni 30.50 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ambapo zaidi ya Shilingi bilioni 18.52 ni za Mishahara na zaidi ya Shilingi Bilioni 11.98 ni za Matumizi Mengineyo.

Huku zaidi ya Shilingi Bilioni 181.95 zinatumika kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ambapo zaidi ya Shilingi bilioni 146.777 ni Fedha za Ndani na zaidi ya Shilingi bilioni 35.176 ni Fedha za Nje.

Akizungumza utekelezaji wa bajeti iliyopita Waziri Nape amesema Mwaka wa Fedha 2022/23 Wizara iliidhinishiwa kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 282.06, Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 26.3 ziliidhinishwa kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi bilioni 255.8 ziliidhinishwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.

Hata hivyo hadi kufikia mwezi Aprili, 2023 Wizara imepokea na kutumia jumla ya Shilingi bilioni 125.1. Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 12.8 sawa na asilimia 48.7 ya fedha za matumizi ya kawaida na Shilingi bilioni 112.3 sawa na asilimia 43.9 ya fedha za mendeleo.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn