logo

IGP WAMBURA ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA SABASABA 2025

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Camillius Wambura leo Julai 6, 2025 ametembelea banda la Wizara ya Katiba na Sheria katika maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2025).

IGP Wambura ametembelea idara mbalimbali katika banda la Wizara hiyo na kupata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Kutoa Taarifa za Haki za Binadamu Bi. Beatrice Mpembo ambaye amempitisha katika idara zote zinazotoa huduma katika Maonesho hayo.

‎Idara hizo ni pamoja na Idara ya Haki za Binadamu, Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma, Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki, Kituo cha Huduma kwa Mteja pamoja na banda la kutolea huduma za Msaada wa Kisheria kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn