logo

MAZAOHUB YAPOKEA UWEKEZAJI MPYA UTAKAOWAWEZESHA WAKULIMA KUPATA HUDUMA KIDIJITALI

Kampuni inayojihusisha na masuala ya teknolojia za kilimo, MazaoHub imepokea uwekezaji mpya kutoka taasisi mbili ambazo ni Elea Foundation na Nordic Impact Funds, uwekezaji huo unalenga kuimarisha huduma za ugani kidijitali na kutengeneza mtandao wa maafisa ugani yaani Uber ya maafisa ugani, ikiwa ni Pamoja na kuzindua jukwaa la masoko ya wakulima kidijitali liitwalo , Cropsupply.com.

.

Akizungumzia kuhusiana na uwekezaji huo Afisa Mtendaji Mkuu wa MazaoHub, Bw. Geophrey Tenganamba amebainisha kuwa utawawezesha wakulima kupata huduma kidijitali kwa usaidizi wa karibu na maafisa ugani ikiwa ni Pamoja na kuwezesha wakulima kuuza Mazao kwa uwazi, kwa faida na kwa uhakika ndani na nje ya Tanzania.

.

Akizungumzia zaidi kuhusiana na namna uwekezaji huo umeisaidia kampuni yake ya Mazao Hub kutekeleza majukumu yake, Tenganamba amebainisha kuwa kampuni hiyo imeanzisha Jukwaa linalowaunganisha wakulima na masoko lijulikanalo kama CropSupply.com. ambalo wakulima, wanunuzi, wasafirishaji na wafanyabiashara wa mazao wanapata taarifa sahihi kuhusiana na upatikanaji wa Mazao kila nchi, kila mkoa na kila Kijiji ikiwa ni Pamoja na kuzalisha repoti ya uzalishaji yaani traceability reports zinazohitajika zaidi na wanunuzi kutoka nje.

.

“Hakika chini ya uwezeshwaji wa Wizara ya Kilimo kampuni yetu ya Mazao Hub ambayo ni kati ya matokeo ya mradi wa BBT imekuwa ikipata uwekezaji kutoka kwa wadau tofauti ambapo kwa sasa uwekezaji huu unaiwezesha kampuni kuyafungua masoko ya wakulima kwa njia ya kidigitali hususan katika kuagiza na kufanya biashara ya mazao kwa chini ya mfumo wa cropsupply.com” amesema Tenganamba.

.

Pia anabainisha zaidi kuwa mfumo huo utawezesha wakulima wa hapa nchini kuuza bidhaa zao nje ya nchi, ambapo kwa sasa mfumo unafanya kazi katika nchi tatu ambazo ni Tanzania, Kenya na Zambia kwa kuwa nchi hizi zinafanya kazi kwa ukaribu zaidi na Tanzania katika sekta ya kilimo.

.

Ameongeza zaidi kuwa kwa kuwa mfumo huo una data za shughuli zote kilimo ambazo zimekuwa zikisimamiwa na MazaoHub kupitia Kliniki zake za kilimo, hivyo mnunuaji anaweza kuona mazao yamelimwaje, akahakiki hatua kwa hatua kupitia mfumo wa ugani wa Mazao Hub. Na hivyo mnunuzi anaweza kujiridhisha juu ya usalama wa mnyororo mzima wa thamani wa mazao kuanzia shambani hadi sokoni.

.

“Hadi sasa wakulima 3,710 wamehusika kama sehemu ya majaribio ya CropSupply.com na kwa mwanzo huu tunaotarajia kuuzindua rasmi, tunategemea kufikia mara 100 zaidi yaani wakulima zaidi ya 370,000 ili kuwezesha biashara salama, ya uwazi, na yenye ushindani barani Afrika” amesema Tenganamba.

.

Katika kuhakikisha ndoto za Mazao Hub ambazo ni kuwa na Afrika inayojitegemea, inayolisha watu wake kwa maarifa na teknolojia zinafikiwa, kampuni hiyo ambayo Februari mwaka huu imeshinda tuzo kama kampuni bora ya teknolojia za Kilimo Barani Africa kwenye shindani la Africa Tech Summit ililofanyika Nairobi, Kenya kutoka na umahiri katika huduma yake ya Kliniki za Kilimo.

.

Huduma za Kliniki za Kilimo na hii mpya ya CropSupply.com ni harakati za kuiwezesha Mazao Hub kuwaunganisha wakulima wa vijijini kwa huduma za ugani kwa kilimo chenye tija na masoko ya kitaifa na kimataifa kwa kutumia data halisi kutoka mashambani ili kuondoa ubabaishaji kwenye biashara ya mazao Afrika.

Wakati Cropsupply.com ikilenga kuiwezesha sekta ya kilimo kidigitali zaidi Kliniki za Kilimo yenyewe hutumia data kuanzia afya ya udongo, afya ya mimea mpaka mavuno kwa lengo la kuongeza mavuno zaidi kwa gharama ndogo ya uzalishaji kwa kutumia data. Hii ni kwa wakulima wadogo, wakulima wa kati mpaka wakulima wakubwa.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn