logo

INJINIA ANNA ATEMBELEA MABANDA YA WADAU WA CHAI NYERERE SQUARE JIJINI DODOMA

Mkuu wa Idara ya Mechanization -Wizara ya Kilimo, Mha. Anna Mwangamilo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Geofrey Mweli (@gerrygeofrey) ametembelea mabanda ya Wadau mbalimbali wa chai wanaoshiriki kwenye Maonesho ya Siku ya Chai Duniani yanayoendelea katika Uwanja wa Nyerere Square.

Akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai Tanzania (TBT), Bi. Beatrice Banzi wametembelea maonesho hayo ambapo wamejionea matukio mbalimbali yanayoendelea.

Pia Mha. Anna alipata wasaha wa kukabidhi zawadi ya mitungi ya gesi kwa washindi 10 wa shindano la kupika chai lililoandaliwa na kampuni ya Maanjumat Group.

Aidha, Katika Maonesho hayo zipo kampuni kadhaa za chai na za watoa huduma ya chai kama Chef Asili, Afritea, Kazi Yetu, Mponde na Shirika la Care.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn