logo

JWTZ YATANGAZA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI VIJANA WA KITANZANIA

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetangaza nafasi za kuandikishwa Jeshini kwa vijana wa kitanzania wenye elimu kuanzia elimu ya Sekondari hadi elimu ya juu.

Hayo yameelezwa leo April 30,2025 na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano (JWTZ) na Msemaji wa JWTZ Kanali Gaudentius Ilonda wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma.

Kanali Ilonda amesema sifa za mwombaji ni lazima awe raia wa Tanzania mwenye kitambulisho cha Taifa,awe na afya nzuri na timamu,mwenye tabia na nidhamu nzuri,hajapatikana na hatia ya makosa ya jinai mahakamani na kufungwa, Cheti halisi Cha kuzaliwa (Original Birth Certificate) Vyeti vya Shule na taaluma.

Vilevile awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza,Chuo Cha Mafunzo au kikosi Cha kuzuia Magendo,awe amehitimu Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT kwa mkataba wa kujitolea au mujibu wa sheria na kutunukiwa Cheti.

Amesema kwa vijana wenye elimu ya kidato cha Nne na kidato cha Sita wawe na umri usiozidi miaka 24,Vijana wenye Elimu ya Stashahada umri usiozidi miaka 26, Vijana wenye elimu ya juu umri usiozidi miaka 27,na Madaktari Bingwa wa binadamu umri usiozidi miaka 35 ya kuzaliwa

Aidha, Taaluma adimu zinazohitajika ni Generall Surgeon,Orthopaedic Surgeon,Urologist Radiologist,ENT Specialist,Anaesthesiologist,Physician, Ophthalmologist, Paediatrician, Obstetrician & Gynaecologist,Ocologis, Pathologist, Psychiatrist, Emergency Medicine Specialist na Haematologist.

Pamoja na Medical Doctor, Dental Doctor, Veterinary Medicine,Bio Medical Engineer,Dental Laboratory Technician, Anaesthetic, Radiographer,Optometry, Physiotherapy na Aviation Doctor.

Aidha Taaluma za Uhandisi(Engineer) ni pamoja na Bachelor of Electronic Engineering, Bachelor of Mechanical Engineering, Bachelor in Marine Engineering, Bachelor in Marine transportation & Nautical Science, Bachelor in Mechanic in Marine Diesel Engine, Bachelor in Aviation Management, Bachelor in Aircraft Accident & Incident Investigation, Bachelor in Meteorology, Air Traffic Management & Aeronautic Engineering bila kusahau Fundi Mchundo Aluminum Welding na Welding & Metal Fabrication.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn