logo

HADI KUFIKIA APRILI 2025,MITUNGI 154,224 IMESAMBAZWA NCHINI -DKT.BITEKO

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau imeendelea kutoa elimu kuhusu umuhimu wa nishati safi ya kupikia pamoja na kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya nishati safi ya kupikia katika Taasisi za Umma na binafsi zinazohudumia zaidi ya watu 100 kwa siku, ikiwemo Jeshi la Magereza, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Shule za Sekondari.

.

"Aidha, zoezi la kusambaza mitungi 452,445 ya gesi ya kupikia (LPG) kwa bei ya punguzo la hadi asilimia 50 liliendelea, na kupitia programu hii jumla ya mitungi 154,224 imesambazwa hadi kufikia Aprili 2025" alisema.

.

Dkt. Biteko ameyasema hayo leo April 28,2025 alipokuwa akiwasilisha Hotuba ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa mwaka 2025/2026 Bungeni jijini Dodoma.

.

Amesema Hatua nyingine zilizochukuliwa ili kuimarisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini ni kuanza utekelezaji wa mradi wa kusambaza majiko banifu 200,000 yaliyotengenezwa kwa teknolojia yenye ubunifu wa kupunguza matumizi ya kuni na mkaa na hivyo kuwezesha kupunguza uharibifu wa mazingira katika maeneo ya vijijini na vijiji-miji.

.

"Hadi Aprili 2025, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeshapata kampuni sita (6) za kusambaza majiko banifu 192,038 katika maeneo ya vijijini na vijiji - miji kwenye mikoa 23 kwa bei ya ruzuku ya hadi asilimia 75" alisema Dkt. Biteko.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn