logo

NEMC YASHUGHULIKIA MALALAMIKO 1,483 KWENYE ENEO LA KELELE NA MITETEMO

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Immaculate Semesi, amesema zaidi ya tani 150 za vifungashio visivyokidhi viwango vilikamatwa, vikataifishwa na kuteketezwa kwa mujibu wa Sheria.

.

Dkt. Immaculate ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Baraza hilo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo Machi 24, 2025 jijini Dodoma.

.

"Suala la udhibiti wa vifungashio vya plastiki ni letu sote, hatuna budi kushirikiana kwa ajili ya kuleta matokeo chanya.

Amesema kwa kipindi cha miaka minne (4), jumla ya kaguzi 9,606 zilifanyika na malalamiko 1,483 yalishughulikiwa hasa katika eneo la kelele na mitetemo.

.

"Uchafuzi wa mazingira ulidhibitiwa katika miradi mikubwa yenye viashiria hatarishi ambapo programu 50 za elimu na vipindi 75 vya uhamasishaji vilifanyika" alisema Dkt. Immaculate.

.

Aidha, amesema Baraza limefanya tathmini ya Ubora wa Maji ya Ziwa Victoria na kuaianisha maeneo yanayotakiwa kupewa kipaumbele katika suala zima la kulinda ubora wa maji kutokana na athari zilizobainika Ziwa Victoria.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn