TIB YAWEKEZA SH.BILIONI 630.3 KATIKA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO NCHINI
Benki ya Maendeleo TIB imeripoti kuwekeza zaidi ya Shilingi bilioni 630.3 katika miradi ya maendeleo yenye athari chanya kwa jamii na uchumi.
.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bi. Lilian Mbassy ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Benki hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo Machi 20, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, jijini Dodoma.
.
Amesema kupitia uwekezaji huo mkubwa zaidi ya ajira mpya 12,547
zimezalishwa kutokana na Benki kufadhili miradi ya muda wa kati na mrefu nchini.
.
“Tunajivunia kutekeleza malengo ya Serikali kwa kuwekeza zaidi ya Shilingi Bilioni 630.3 katika miradi ya maendeleo ambazo zimezalisha zaidi ya ajira mpya 12,547,” alisema Mbassy.
Amesema Benki hiyo itaendelea kukuza mtaji wa Benki kwa kushirikiana na taasisi za katika miradi ya maendeleo ambazo zimezalisha zaidi ya ajira mpya 12,547.
.
Aidha, Lilian amesema Serikali katika kutekeleza sera na mikakati ya kitaifa ili kuongeza kasi ya maendeleo,TIB kama benki ya maendeleo ni taasisi ya kisera ambayo ina jukumu la kuunga mkono juhudi za Serikali Katika Kutekeleza sera na mikakati mbalimbali.
.
“Katika mwaka 2025 Benki vipaumbele vyake vimejikita katika kuunga mkono juhudi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkono juhudi za Serikali katika kutekeleza sera na mikakati ya kitaifa hususani kwenye pamoja na kutekeleza vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Sita" alisema.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

