THAMANI YA UTAJIRI WA DANGOTE YAPANDA HADI DOLA BILIONI 23.8 -FORBES
Bilionea maarufu kutoka nchini Nigeria, Aliko Dangote, inaripotiwa ya kwamba utajiri wake umepanda hadi kufikia dola Bilioni 23.8 karibia mara mbili ya thamani aliyokuwa nayo mwaka jana 2024.
.
Mnigeria huyo mwenye umri wa miaka 67, amerejea katika orodha ya 100 bora zaidi tangu mwaka 2018, hii ni kulingana na Orodha ya Mabilionea ya wakati halisi ya jarida la Forbes la nchini Marekani.
.
Bilionea Dangote amevunja ukiritimba wa Serikali yake kwa kujenga kiwanda kikubwa zaidi cha kusafisha mafuta barani Afrika na mpaka hadi sasa, ni yeye pekee ndiye amevuna thawabu.
.
Baada ya miaka 11, uwekezaji wa dola bilioni 23 na maumivu ya kichwa yasiyohesabika, Kiwanda cha Kusafisha Mafuta cha Dangote hatimaye kilianza kufanya kazi mwaka jana.
.
Kikiwa kwenye kampasi yenye ukubwa wa ekari 6,200 katika eneo huru la Lekki nchini Nigeria takribani saa moja nje ya Lagos, kiwanda hicho kilichakata takribani mapipa 350,000 ya mafuta ghafi kwa siku (b/d) katika nusu ya pili ya 2024.
.
Dangote amesema kiwanda cha kusafisha mafuta ni sehemu ya dhamira kubwa zaidi: Anataka kuifanya Nigeria, mojawapo ya wazalishaji wakubwa wa mafuta ghafi duniani, kuwa mzalishaji wa bidhaa za petroli iliyosafishwa ili kuiruhusu kushindana na viwanda vya kusafishia mafuta vya Ulaya na kusambaza petroli kwa Wanigeria.
.
Majaribio ya awali ya serikali ya Nigeria kujenga na kuendesha mitambo mikubwa ya kusafisha yaliishia bila mafanikio, na kuwaacha watumiaji wa Nigeria na biashara kutegemea uagizaji wa petroli, hasa kutoka Ulaya.
.
Dangote anataka kutoa mwongozo wa maendeleo ya viwanda barani Afrika.
.
"Lazima tujenge taifa letu sisi wenyewe, Tunapaswa kujenga bara letu sisi wenyewe, sio kutegemea uwekezaji kutoka nje" alisema.
"Afrika imekuwa mahali pa kutupia bidhaa zilizomalizika," Dangote anahoji, na kiwanda chake cha kusafisha kinawakilisha "hatua muhimu katika kuhakikisha kwamba Afrika ina uwezo wa kusafisha mafuta yake ghafi, na hivyo kutengeneza utajiri na ustawi kwa wakazi wake wengi."
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

