WANACHAMA 2,439 WA ACT WAZALENDO WAJIUNGA NA CCM MKOA WA KUSINI PEMBA
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewapongeza na kuwakaribisha Wanachama 2,439 wa chama cha ACT Wazalendo kwa uamuzi wa kujiunga na CCM kwani wamefanya uamuzi sahihi na kuwaahidi Ushirikiano wa kiwango cha juu.
.
Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi Mauwani, Kiwani Mkoa wa Kusini Pemba Katika Mkutano Maalum wa Mapokezi yake baada ya Kuteuliwa hivi Karibuni kuwa Mgombea wa Urais wa Zanzibar.
.
Amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya wana CCM kutojitokeza kupiga kura wakati wa uchaguzi jambo linaloipunguzia kura za ushindi chama hicho.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameipongeza UWT kwa kazi nzuri walioifanya ya Uhamasishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura na kuiagiza kuendelea na mwamko huo.
.
Kwa upande mwingine, Dkt.Mwinyi amezisisitiza Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi kuwahamasisha Wanachama na Wananchi kujiandikisha na kujitokeza kwa Wingi kupiga Kura ili CCM ishinde kwa Kishindo.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

