SERIKALI INAKWENDA KUJENGA SHULE ZA UFUNDI KILA HALMASHAURI NCHINI
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe.Deogratius J.Ndejembi Amesema Serikali inakwenda Kujenga Shule za Ufundi Katika Kila Halmashauri ya Nchi Yetu ambayo ilikosa Shule Ya VETA.
.
"Haya Ndio Mageuzi ambayo Dkt.Samia Suluhu Hassan Anayafanya Katika Sekta ya Elimu kwenye Nchi Yetu Hii Ya Tanzania. Nasema Ni Katika Halmashauri ambazo Hazikupata VETA, Ni Sera Ya Serikali Kuhakikisha VETA zinakwenda Katika Halmashauri Zote Nchini Lakini Awamu Hii ya Kwanza zilipata Halmashauri 63 ambazo Zilienda kiwilaya".
.
Ndejembi Ameyasema Hayo Leo Mei 14,2023 Jijini Dodoma Alipokuwa Akifunga Kongamano la Sera Na Mitaala Ya Elimu lililofanyika Katika Ukumbi Wa Jakaya Kikwete Convertion Center.
.
Amesema Shule Hizo zitakazokwenda kujengwa zitatoa Mafunzo ya Amali ambayo Yatawawezesha Vijana hapa Nchini wanaohitimu Katika Shule Hizo.
.
"Kwanza Kuwa Na Ujuzi Lakini Pia Watatoka Na Cheti ambacho ni Sawa Sawa Na Kile wanachokipata wenzao Katika VETA ambazo zipo Katika Maeneo Mengine ya Halmashauri Hizi hapa Nchini.
.
"Haya Ni Mabadiliko Na Mageuzi makubwa Sana na Yote Haya yanatokea Katika Awamu Hii Ya Sita Ya RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan" Amesema Ndejembi.
.
Aidha, Naibu Waziri huyo Amewataka Wadau Wa Elimu Kuhakikisha wanatoa Sapoti Kubwa Sana Kwa Wizara Ya Elimu.
.
"Sapoti Yetu Itawezesha Mageuzi Haya Kutokea Katika Taifa Letu, Itafanya tuweze Kuboresha Mambo Mbalimbali Katika Elimu".
.
Nae Waziri Wa Elimu, Sayansi Na Teknolojia Mhe. Prof.Adolf Mkenda Amesema Mitaala Hiyo Tayari Bajeti yake Imeshatengwa Kuanza Kuwaanda Walimu na Kazi Itaanza Sasa Hivi.
.
Mkenda Amesema Katika Mafunzo Ya Amali Watu hawapaswi Kuyadharau Na Ndio Maana Wameanza na Vyuo Vya Ufundi hivyo Mafunzo hayo Sio ya Watu waliofeli.
.
Nae Mwenyekiti Wa Kamati Ya Kudumu Ya Bunge Ya Elimu, Utamaduni Na Michezo Mhe.Prof. Kitila Mkumbo Amesema Kutokana Na Umakini na Uhodari Wa Waziri Mkenda Katika Wizara Hiyo, Hivyo anaamini Suala la Sera Na Mitaala Ya Elimu Mipya litakwenda Vizuri Na Katika Miaka 5 au 10 ijayo Elimu Yetu itakuwa imebadilika.
@ortamisemi
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

