WAHITIMU JKU ZANZIBAR WATAKIWA KUWA MABALOZI WAZURI KUPITIA MAFUNZO WALIYOYAPATA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Masoud Ali Mohamed amesema kuwa Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) limefanya kazi kubwa ya kuwafanya vijana hao kuwa wamoja wenye kuenzi mila na desturi za mtanzania.
Mhe. Masoud ameyasema hayo alipokuwa akihitimisha Mafunzo ya Vijana wa JKU mkupuo 069 na kundi maalum 070 la Vijana wa Ufundi wa JKU katika Kikosi Cha KAMA kilichopo Zanzibar Mkoa wa mjini Magharibi.
Amefafanua kuwa, Mafunzo waliyoyapata vijana hao yatawapa uwezo mkubwa wa kukabiliana na maisha yao ya kila siku na wayazingatie kwani yanafaida kubwa kwa Taifa.
"Mkawe mabalozi wazuri wa JKU kwa Mafunzo mliyo yapata kwa kipindi chote Cha miaka miwili mliyo kuwepo hapa". alisema.
Ameongeza kuwa kupitia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar endapo kutatokea fursa za ajira itatoa kipaumbele hasa kwa vijana waliopata Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU).
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

