logo

RASIMU YA SERA NA MITAALA MIPYA YA ELIMU YAKAMILIKA

WAZIRI Wa Elimu,Sayansi Na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Amesema Rasimu Ya Sera Ya Elimu Na Mafunzo Ya 2014 Toleo La 2023 imeshakamilika Na Rasimu Ya Mitaala Mipya Ya Elimu Ya Awali, Msingi, Sekondari Na Vyuo Vya Ualimu ambayo inakidhi Maelekezo Ya RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan Nayo imeshakamilika.

.

Mkenda Ameyasema hayo Leo Mei 09,2023 Alipokuwa Jijini Dodoma Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Katika Ukumbi Wa Danida.

.

Amesema Serikali imeamua Kutoa Rasimu Hizo Hadharani Ili Kupata Maoni ya Mwisho Na Wangependa Kuyapokea Maoni Hayo Ifikapo Tarehe 31 Mwezi Mei 2023 ambapo itakuwa Ni Mwisho Wa Kupokea Maoni.

.

"Mwanzoni Tulipokea Maoni Bila Kuwa Na Rasimu, Tuliyapokea Na Kuyachambua Halafu Tukayafanyia Kazi .. Tumeyachakata Maoni Haya, Tumefanya Uchambuzi Wa Kitaalamu, Tumejifunza Kutoka Nchi Mbalimbali.

.

"Tumetengeneza Rasimu Sasa Umma Wa Watanzania Utaziona Rasimu Hizo Ili watolee Maoni kwenye Rasimu Hizi ambazo Baada ya Kuzingatia Maoni tutaingiza Kwenye Michakato ya Maamuzi" Amesema Mkenda.

.

Mkenda Amesema Kesho Mei 10,2023 Watakuwa Na Semina Na Wabunge Wote kuwapitisha Kwenye Rasimu Hizo za Mapitio Ya Sera Na Mitaala Mipya.

.

Aidha, Mkenda Ametoa Wito Kwa watanzania Wote Kupitia Rasimu Hizo na Kutoa Maoni Yao, Pia Amesema Rasimu Hizo zinapatikana Katika tovuti Ya Wizara Ya Elimu Sayansi Na Teknolojia, Idara Ya Habari maelezo Na Ya Taasisi Ya Elimu Tanzania.

Naye Katibu Mkuu Wa Wizara Hiyo Mhe. Prof. Carolyne Nombo Amesema Suala Hilo La Rasimu Lipo Ndani Na Nje Ya Nchi na Kwa watanzania Wanaoishi Nje (Diaspora) wanakaribishwa Kushiriki Katika Mjadala ambapo kutakuwa Na Utaratibu Maalum.

.

"Diaspora Wao Pia Wanakaribishwa Kwa Namna Ya Pekee Lakini Pia Tufahamu Ni Kitu ambacho ni Cha Kimataifa. Mtaala unakuwa Ni Benchmark Kwahiyo Watanzania Wenzetu waliopo Huko Watatusaidia Kujua Kuna Nini na Kutupa Maoni Namna ya Kuboresha Mitaala Hii Kulingana Na Uzoefu Wa Nje Nyingine" Amesema Nombo.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn