SIMBACHAWENE ATEMBELEA BANDA LA DUWASA MAONESHO WIKI YA UTUMISHI WA UMMA
Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene leo Juni 19, 2024 ametembelea Banda la Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) katika Uzinduzi wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
Waziri Simbachawene ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa maonesho hayo amewataka watumishi wa Umma kutimiza wajibu wao kwa kwenda na kasi ya utendaji ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwatumikia wananchi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph katika kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Mamlaka za maji nchini kuanza kutumia mita za maji za malipo ya kabla (pre-paid meter) tayari DUWASA imeshawafungia mita hizo wateja 1500 katika maeneo mbalimbali yanayohudumiwa na DUWASA ya Jiji la Dodoma, Bahi, Kibaigwa, Kongwa na Chamwino.
DUWASA inashiriki Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanza Juni 16, 2024 na yatafikia kilele chake Juni 23, 2024.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

