DORIS MOLLEL FOUNDATION YAIPONGEZA SERIKALI OMBI LA KUONGEZA SIKU ZA LIKIZO KWA WANAWAKE WANAOJIFUNGUA WATOTO NJITI NCHINI
Taasisi ya Doris Mollel imetoa pongezi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kwa uamuzi wake wa kukubali ombi la kuongeza siku za likizo kwa wanawake wanaojifungua watoto njiti hapa nchini katika Sherehe za Kilele cha Mei Mosi Kitaifa, zilizofanyika jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bi.Doris Mollel ametoa pongezi hizo leo Mei 03,2024 alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar Es Salaam ambapo amesema Taasisi ya Hiyo ilianzisha wazo hilo na inatambua mchango wa wadau mbalimbali walioshirikiana na Taasisi Mbalimbali katika kuanzisha Mchakato wa kuiomba Serikali kufanya marekebisho kwenye sheria ya likizo ya uzazi ambao ulianza mwaka 2017, ambao ni pamoja na Wataalam wa Afya, Wazazi wa watoto njiti, Wataalam wa Sheria, Chama cha Madaktari wa Watoto Wachanga.
"Hivi karibuni Serikali ilibainisha kwamba kuanzia sasa iwapo mfanyakazi atajifungua mtoto njiti,kipindi cha uangalizi maalum hakitahesabika kama likizo ya uzazi, na likizo ya uzazi itaanza tu baada ya kumalizika kwa kipindi hicho
cha uangalizi, kadiri madaktari watakavyothibitisha".
Vilevile, mfanyakazi husika ataruhusiwa kutoka kazini saa 7:30 mchana kila siku kwa muda wa miezi sita baada ya kumalizika kwa likizo ya uzazi,
ili kumpa fursa ya kwenda kunyonyesha.
Mkurugenzi huyo amesema Taasisi hiyo inatambua kwa dhati mchango usiopimika wa wadau wa maendeleo,hasa Women Fund Tanzania Trust, Asas Group, na Segal Family Foundation.
"Vilevile, tunatoa shukrani zetu za dhati kwa waandishi vinara wa watoto njiti, ambao wamesaidia kusambaza na kupigania ajenda mbalimbali zinazohusu watoto njiti.
.
"Taasisi ya Doris Mollel iko tayari katika kushiriki kwa kina katika hatua zote zinazofuata za kuendeleza na kuhakikisha uamuzi huu unajumuishwa katika Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, kwa ushirikiano thabiti na wadau wetu, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) na Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE)" alisema Doris Mollel.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

