logo

NELSON MANDELA NA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA ZADHAMIRIA KULETA MABADILIKO KWENYE JAMII

Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kwa kushirikiana na Shirika la Posta Tanzania zimekubaliana katika kuleta mabadiliko ya pamoja kwa jamii katika eneo la utoaji huduma kidigitali.

Hayo yamesemwa na Makamu Mkuu wa Taasisi Profesa Maulilio Kipanyula wakati wa kikao na Postamasta Mkuu Bw. Maharage Chande alipofanya ziara ya kikazi tarehe 8 Aprili, 2024 katika kampasi ya Tengeru Arusha.

“Ushirikiano huu utasaidia katika kuboresha utoaji wa huduma za Posta kwa jamii kidigitali, ukizingatia taasisi yetu imejikita katika kufanya tafiti hivyo kupitia shule ya Sayansi na Uhandisi wa Ukokotoaji na Mawasiliano haya yote yatawezekana “anasema Prof. Maulilio.

Kwa Upande wake Postamasta Mkuu Bw. Chande ameeleza kufurahishwa na hatua hiyo, ambapo kwa pamoja wataweza kuboresha huduma za Posta kwa kuzifanya kuwa za kidigitali ili kuifikia jamii kubwa ya Tanzania.

Naye Amidi wa Shule Kuu ya Sayansi na Uhandisi wa Ukokotoaji na Mawasiliano (CoSCE) Dkt. Mussa Dida ameeleza kuwa, wako tayari kushirikiana kwa karibu na Shirika hilo kupitia wataalamu waliopo katika kutoa utaalamu wa namna ya kuboresha huduma za posta nchini.

Katika ziara hiyo, Bw. Maharage Chande alipata fursa ya kutembelea Kituo Atamizi (Incubation Center) na kompyuta yenye uwezo mkubwa wa kuchakata data kwa kasi kubwa (Param Kilimanjaro Super Comput

er).

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn