logo

WAZIRI MKENDA: MTOTO ASIRUDISHWE NYUMBANI KISA HAJACHANGIA CHAKULA SHULENI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ameelekeza kuwa Wanafunzi wote nchini wasirudishwe nyumbani kisa hawajachangia chakula shuleni.

.

Prof.Mkenda ameyasema hayo leo April 05,2024 alipokuwa akifunga Mkutano wa Mwaka wa Pamoja wa Tathmini ya Sekta ya Elimu uliofanyika jijini Dodoma.

.

Amesema maana ya 'ELIMU BILA ADA' ni kwamba mtoto aende shuleni akasome lakini michango ya aina yoyote ile isiwe kikwazo kwa mwanafunzi kushindwa kupata elimu anayoistahili.

.

"Tuendelee kuhamasisha wazazi watoe michango ya chakula na michango mingine, ila mtoto asirudishwe nyumbani kisa hajachangia chakula"alisema Mkenda.

.

Waziri Mkenda amesema hakuna mtu yeyote anakataza kijiji,mtaa,Serikali, halmashauri kuchukua hatua dhidi ya mzazi ambaye hachangii chakula shuleni,lakini hakuna adhabu inayoruhusiwa ya kumtoa mwanafunzi shuleni kwa sababu mzazi kakataa kufanya kile ambacho jamii imekifanya.

.

Kwa upande mwingine,Mkenda amewataka watumishi wa sekta ya Elimu kuwahudumia vizuri walimu pale ambapo wanahitaji msaada kutoka kwao.

.

Aidha,Prof.Mkenda amewaomba na kuwataka wadau wa Maendeleo sekta ya Elimu kuhakikisha wanatoa misaada inayoendana na jinsi sera ya Elimu inavyokwenda.

.

"Hatutaki kutapanya tapanya juhudi,tunataka tuzielekeze kule ambapo tunakwenda, Project yoyote tutakayo kubaliana na Shirika lolote lile tungependa kuliangalia linaendana vipi katika safari hii ya mageuzi ya Elimu" alisema Prof.Mkenda.

.

Naye Kamishna wa Elimu Tanzania Dkt.Lyabwene Mutahabwa amesema katika majadiliano ya mkutano huo wameafikiana ya kwamba,ifike mahali Serikali ione umuhimu wa kutunga Sheria ya kuwalazimisha Wazazi kuchangia chakula shuleni.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn