logo

WATUMIAJI WA MIONZI HAKIKISHENI MNAKUWA NA VIBALI VYA KUTUMIA MIONZI NCHINI - MKURUGENZI TAEC DKT.NGAILE

Mkurugenzi wa Kinga ya Mionzi wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania TAEC Dkt.Justin Ngaile amewataka watumiaji wa vyanzo vya mionzi nchini kutii sheria ya Nguvu za Atomu namba (7) ya mwaka 2003 kwa kuhakikisha wanakuwa na vibali vinavyowawezesha kuingiza vyanzo vya mionzi,kumiliki, kutumia na kusafirisha vyanzo vya mionzi.

.

"Kama mtu atakwenda kinyume na taratibu zetu, kuna hatua kali zitachukuliwa dhidi ya mhusika" alisema.

.

Dkt.Ngaile ameyasema hayo mara baada ya kufanya ukaguzi katika hospitali ya wilaya ya Chato na Hospitali ya Rufaa ya Chato mkoani Geita.

Mkurugenzi Dkt.Ngaile amesisitiza matumizi ya mionzi nchini ni lazima yasimamiwe vizuri ili kuwalinda wananchi,wafanyakazi na mazingira kwa ujumla.

.

Katika Ukaguzi uliofanyika mkoani Tanga katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bombo, Mkaguzi Mwandamizi wa Mionzi wa TAEC Bw.Lazaro Meza amesema zoezi la ukaguzi linaendana sambamba na kuwahamasisha wadau kutumia mifumo ya Tehama katika uombaji wa vibali vya umiliki wa vyanzo vya mionzi.

.

Aidha,Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania Bw.Peter Ngamilo amesema TAEC inaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili wafahamu faida na madhara ya mionzi.

.

Tume hiyo inaendelea na zoezi la ukaguzi wa matumizi ya mionzi nchini kwa lengo la kujiridhisha kama matumizi ni salama katika maeneo ya hospitalini,viwandani,vituo vya utafiti, migodini,bandarini,viwanja vya ndege pamoja na katika ujenzi wa barabara na reli.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn