WAZIRI MKUU MAJALIWA AZITAKA HALMASHAURI KUWEKA MPANGO WA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA MATUMIZI YA ARDHI
WAZIRI MKUU Mhe.Kassim Majaliwa amezielekeza Halmashauri zote zinazotekeleza mradi wa Mpango wa Matumizi ya Ardhi ya Vijiji kuandaa mpango wa ufuatiliaji na tathmini ili kupima ufanisi wa utekelezaji wa mradi huo.
Mhe.Majaliwa ametoa maelekezo hayo leo Ijumaa, Machi 22, 2024 wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa Kujadili Utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi uliofanyika wilayani Ruangwa mkoani Lindi.
Waziri Mkuu pia amezielekeza Halmashauri zote ziandae mpango mahsusi wa kupata suhulu ya migogoro inayohusu mipaka ya vijiji.
“Lengo la Serikali ni kupima ardhi yote nchini ili wananchi wakiwepo wanavijiji waweze kuitumia katika kufanya shughuli za kiuchumi, Wenyeviti wa Halmshauri hakikisheni mnatoa ushirikiano kwa Timu inayotekeleza mradi ili mapungufu yaliyopo yapatiwe suluhu.
“Nisisitize Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wenyeviti na Watendaji katika vijiji washiriki kikamilifu kuwafikia wananchi na kuwaelimisha umuhimu wa matumizi sahihi ya ardhi, ili waweze kunufaika pamoja na kupata hati miliki za ardhi wanayoimiliki” alisema Waziri Mkuu.
Aidha, Majaliwa amewataka Watalaam wa sekta ya ardhi, kushirikiana na viongozi wa Serikali za mitaa na vijiji katika hatua zote za utekelezaji wa mradi.
.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda, amesema mradi huo unategemea kutekelezwa katika Halmashauri za Wilaya zilizoko kwenye mpaka wa kimataifa wa nchi, Wilaya zenye migogoro mingi ya matumizi ya ardhi na Wilaya zenye fursa kubwa za kiuchumi.
Kwa upande wake Meneja wa Mradi Vijijini Joseph Osena, amesema kuwa Mradi huo wa Uboreshaji usalama wa milki za Ardhi unaenda kutatua changamoto nyingi za ardhi ambazo zimekuwa zikiyakumba maeneo mengi nchini.
Naye Diwani wa Kata ya Ruangwa Halima Mponda, ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maeneo ya Makazi kwa juhudi inazozifanya katika kupima vijiji hali ambayo inaenda kumaliza migogoro mingi iliyokuwa inatokea.
Mradi wa uborshaji wa usalama wa miliki za Adhi (LTIP) unasimamiwa na Wizara ya Adhi Nyumba na Mandeleo ya Makazi ukiwa na kauli mbiu isemayo; “Usawa wa Kijinsia katika Umiliki wa Ardhi katika ustawi wa Jamii”.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

