logo

MKENDA: TUJENGE UCHUMI WETU KWA KUTUMIA SAYANSI NA TEKNOLOJIA

WAZIRI Wa ELIMU Sayansi Na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda Amesema Kama Tanzania Tunataka Kujenga Uchumi Wa Kitaifa Basi Hatuwezi Kujenga Uchumi Huo Kwa Maneno Bali Tunapaswa Kufanya Kwa Vitendo Na Kwa Kutumia Sayansi Na Teknolojia Ili Kuongeza Tija Katika Uzalishaji Wetu Hapa Nchini.

.

Mkenda Ameyasema hayo Leo April 28,2023 Alipokuwa Akifunga Rasmi Kilele Cha Maonesho Ya Wiki Ya Ubunifu Kitaifa 2023 yaliyofanyika Katika Uwanja Wa Jamhuri Jijini Dodoma.

.

Amesema Serikali Ya Awamu Ya Sita Ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeongeza Sana Uwekezaji Katika mambo Ya Sayansi, Teknolojia Na Ubunifu Ili Tuweze Kufika Mbali Kiuchumi Zaidi.

.

"Tumeanza Kuhimiza Vijana Wetu waanze Kusoma Masomo Ya Sayansi Kwa Sababu Wakifanya Vizuri Katika Masomo Hayo, Wakienda Kidato Cha Sita wanapata SAMIA SCHOLARSHIPS.

.

"Ili Tuweze Kuwa Na Wana Sayansi wengi Zaidi, Ili watakapoenda Kufanya Shughuli za Kisayansi, Watatusaidia Kuendeleza Teknolojia Na Baada Ya Teknolojia Watatusaidia kwenda Kwenye Ubunifu" Alisema Mkenda.

.

Aidha, Mkenda Amesema Baadhi Ya Vyuo Vikuu hapa Nchini vimekuwa vikiwaza Ya Kwamba Tatifi zinazofanywa Lengo lake Kubwa ni Kutengeneza Hela Kwa Vyuo Sio Kweli, Kazi Ya Tafiti ni Kutoa Tafiti Nje Na Kuchapisha Na Kutuletea Ujuzi ambayo itatusaidia Katika Kutuletea Teknolojia na Baadae Ubunifu.

.

Nae Mwenyekiti Wa Kamati Ya Kudumu Ya Bunge Ya Elimu, Utamaduni Na Michezo Mhe. Husna Sekiboko Ameipongeza Wizara Ya Elimu, Sayansi Na Teknolojia Kwa Kuendeleza Ubunifu Katika Nchi Yetu Jambo ambalo Ni Kubwa Mno.

.

Sekiboko Ametoa Rai Kwa wazazi Na Walezi Vipaji Vinaonekana Tangu Mtoto akiwa Mdogo hivyo wanapaswa kuisaidia Wizara ya Elimu Kuibua Vipaji, Kuona Watoto Ambao Wana Elimu Ya Ugunduzi wanaripotiwa Kutoka Shule Mbalimbali Ili kuvitambua Vipaji na Baadae kuviendeleza.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn