WAZAZI,WALEZI CHANGIENI CHAKULA SHULENI ILI WATOTO WAPATE LISHE BORA -DKT.FRANKLIN RWEZIMULA
Kufuatia maadhimisho ya Siku ya Afrika ya Chakula Shuleni ambapo kitaifa yamefanyika leo jijini Dodoma, jamii kwa kushirikiana na wazazi pamoja na walezi wametakiwa kuendelea kuchangia chakula ili watoto wao waweze kupata mlo kamili hasa wa mchana kipindi wanapokuwa shuleni.
Akimwakilisha Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof.Adolf Mkenda,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt.Franklin Rwezimula amesema kupatikana kwa lishe shuleni kumeleta matokeo makubwa kwani imesaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi na pia imepunguza tabia ya utoro shuleni kwa baadhi ya wanafunzi.
.
"Kama mnavyotambua Serikali imetoa juhudi kubwa sana katika utoaji wa elimu bila ada na ili mtoto aweze kufaulu vizuri lazima apate chakula, na katika utoaji wa chakula wadau mbalimbali wanashiriki wakiwemo wazazi,walezi, mashirika na taasisi mbalimbali.
.
"Tunamshukuru Mhe.Rais kwa kuhamasisha ushiriki wa watanzania wote kwa kushirikisha wakuu wa mikoa, kwa kuwasainisha mkataba ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika usimamizi wa upatikanaji wa chakula kwenye mikoa yao" alisema Dkt.Franklin.
Aidha,Dkt.Franklin amesema hali ya upatikanaji wa chakula shuleni inaridhisha lakini bado haitoshi kulingana na mahitaji na Serikali itaendelea kuwa bega kwa bega na watanzania wote ili kuhakikisha adhma ya serikali inafanikiwa kwa asilimia 100%.
Nae Mratibu wa masuala ya lishe kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mwalimu Grace Shilelingo amesisitiza suala la lishe bora shuleni kwa lengo la kuongeza na kuimarisha usikivu wa wanafunzi darasani.
.
Aidha,Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Global Communities linalotekeleza mradi wa 'PAMOJA TUWALISHE' mkoani Dodoma na Mara Bi.Vicky Macha amesema shirika hilo limekuwa likitekeleza mradi wa utoaji chakula shuleni kwa takribani miaka 10 kwa mikoa hiyo,hivyo anafurahi kushiriki katika maadhimisho hayo.
.
"Tunafurahi kuona tunashirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Elimu pamoja na ORTAMISEMI katika kuhakikisha lengo hili linafikiwa kwa ajili ya maendeleo ya baadae na tunatimiza kuendelea kushirikiana kwa pamoja katika mambo mengi mbalimbali" alisema Macha.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

