logo

KIPANYULA: TAEC ONGEZENI UWEKEZAJI KWENYE UTAFITI

WITO Umetolewa Kwa Tume Ya Nguvu Za Atomiki Tanzania (TAEC) Kuongeza Uwekezaji Kwenye Utafiti Hasa Katika Eneo la Sayansi Na Teknolojia Ya Nyuklia Ili kuweza Kufika Mbali Zaidi.

.

Hayo Yamesemwa Na Mkurugenzi Wa Idara Ya Sayansi, Teknolojia Na Ubunifu Kutoka Wizara Ya Elimu, Sayansi Na Teknolojia Prof.Maulilio Kipanyula Leo April 27,2023 Jijini Dodoma Alipokuwa Akizungumza Na Waandishi Wa Habari ikiwa Ni Siku Maalum Ya Tume Hiyo.

.

Kipanyula Amesema Ili Mtu Aweze Kubuni au Kuzalisha Ubunifu Katika Eneo Hilo La Sayansi Ya Nyuklia Ni Lazima TAEC wawekeze Kwenye Ubunifu.

.

"Najua Mmeshafanya Uwekezaji Kwenye Kutoa Scholarships Kwa Ajili Ya Wanafunzi Wa Shahada ya Kwanza, Masters au PHD Na Angalie Hasa Upande Huu Wa Utafiti Kama Rasilimali Zinaruhusu ni Muhimu Kuanza Kujenga Uwezo Na Hii Itatuwezesha kuzalisha Ubunifu Na Teknolojia Zaidi" Amesema Kipanyula.

.

Mkurugenzi Huyo Amesema Ili Waweze Kufika Mbali Zaidi Katika Teknolojia, Tume Hiyo inatakiwa Kushirikiana na Kampuni Mbalimbali Hasa Katika Eneo la Nyuklia.

.

"Kampuni zinazohusiana na Nyuklia, Uranium Nk. Jinsi Tunavyokwenda Mbele Tunatamani Makampuni mengi Zaidi waweze kuungana Nasi Kwenye Eneo la Teknolojia" Amesema Kipanyula.

.

Nae. Mkurugenzi Mkuu Wa TAEC Prof. Lazaro Busagala Amesema Kwenye Mpango Mkakati tayari wameshaidhinisha Scholarship Katika Mpango Ule Wa SAMIA SCHOLARSHIP Ambao utasababisha Ubunifu Zaidi Kwa Sababu watakuwa Wanachukua Vijana Ambao wamefanya Vizuri Zaidi Katika Shahada Zao za Kwanza.

.

"Kuanzia Mwaka Huu Tunatarajia kupeleka Vijana 5 Na Mwaka Ujao tutapeleka Vijana 5 na Mwaka Mwingine hivyo hivyo Wakati Huo Huo Kuna Wengine Ambao watapewa ufadhili wakiwepo hapa Hapa Nchini Na Jumla Katika Miaka 3 wanatajia Kutumia Bilioni 2.6 Kuhakikisha Kwamba tunatengeneza Wabunifu Zaidi" Amesema Busagala.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn