WAZIRI MKENDA: TUTAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA ELIMU KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ametoa wito kwa watoto wenye mahitaji maalum ambao wanahitaji msaada maalum kwa ajili ya kusoma watoe taarifa katika wizara ya elimu,Sayansi na Teknolojia ili waweze kusaidiwa.
.
"Mwaka huu tumegawa vifaa kwa wanafunzi wenye mahitaji kwahiyo ningependa kama kuna wenye changamoto tupate taarifa Tanzania nzima, watoto wenye mahitaji maalumu wanaohitaji msaada maalum kwa ajili ya Kusoma watoe taarifa kwenye wizara yetu" amesema.
.
Prof.Mkenda ameyasema hayo leo Oktoba 11,2023 alipokuwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika jijini Dodoma katika Shule ya Sekondari ya wasichana Msalato.
.
Amesema wanakwenda kufanya tathmini hasa ya watoto wa kike walioacha masomo kwa sababu ya ujauzito na kurudi mashuleni, kuona mafanikio na changamoto tulizonazo ili kuangalia namna bora zaidi ya kuhakikisha kwamba wanatekeleza maelezo ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
.
"Kwenye hilo naialika UNICEF kuja kushirikiana na wizara yetu katika kufanya utafiti wa kufuatilia wale wote ambao wamerudi,mmoja mmoja kwa kumuhoji kuangalia mazingira, mafanikio, changamoto na mapendekezo ya namna bora zaidi ya kutekeleza maelekezo haya ya Rais wetu" amesema Mkenda.
.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya elimu,utamaduni na michezo Mhe.Husna Sekiboko ameahidi kwa niaba ya Serikali, mhimili wa Bunge na kamati yao hawatakuwa kikwazo katika kufanikisha yale yote ambayo Serikali inayapanga kwa ajili ya kuendeleza na kumlinda mtoto wa kike nchini.
.
Aidha, Sekiboko amewahimiza wazazi,walezi, wanafunzi na jamii kwa ujumla kwenda kuwa mabalozi wa kulinda maadili kwani mmomonyoko wa maadili hautofanikisha ndoto ya mtoto wa kike au hata duniani kwa sababu wengi wanakwama.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

