TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUNUNUA MIFUMO YA TEHAMA YA e-GA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.George Simbachawene amezitaka taasisi za Serikali kununua mifumo mbalimbali inayotengenezwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) ili kuhakikisha Serikali inatumia fedha zake kwenye shughuli nyingine badala ya kutumia fedha kununua mifumo Kutoka nje.
.
"Zipo baadhi ya Taasisi za Serikali ambazo zinanunua Mifumo, wakati Sisi Taasisi yetu ya e-GA inabuni na kujenga mifumo mbalimbali. Rai yangu kwa Taasisi hizo Badala ya kuendelea kununua mifumo ambayo inatumia fedha nyingi Sana za wananchi basi waje e-GA" amesema.
.
Simbachawene ameyasema hayo leo Septemba 18,2023 alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea kituo cha Utafiti, Ubunifu na uendelezaji Mifumo cha Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kilichopo Chuo Kikuu Cha DODOMA Ndaki ya CIVE.
Amesema matumizi ya TEHAMA ndio muhimili wa mapinduzi ya Nne ya Viwanda, pamoja na matumizi ya TEHAMA, Ubunifu ni moja ya nyanja Muhimu Sana katika kuendeleza na kuharakisha ukuaji wa uchumi wa kidijitali nchini Tanzania.
.
Simbachawene Amesema wananchi wanapaswa kuelewa tupo kwenye ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia na lazima tutumie mifumo ya TEHAMA hivyo wanafunzi waliopo kwenye kituo hicho wanapaswa kuhamasisha wananchi waweze kutumia mifumo hiyo.
.
"Mfano Mfumo wa e-Mrejesho upo lakini nadhani watumiaji sio wengi sana ni vizuri tukahamasisha wananchi mbalimbali waweze kuingia kwenye mifumo hii ili waweze kuwasiliana na Serikali yao" amesema Simbachawene.
.
Waziri huyo amesema juhudi za Serikali kujiimarisha kwenye eneo la TEHAMA ni za kipaumbele na hivyo jitihada za kuboresha Utafiti,Ubunifu zinaendelea ikiwa pamoja na kuwa na mazingira ya kuweza kuchukua vijana wengi zaidi wenye vipaji na wabunifu kwenye eneo la TEHAMA kuweza kufanya majaribio na kujiendeleza kwa vitendo.
.
Aidha, Simbachawene amewapongeza wanafunzi hao kwa ubunifu mkubwa wanaoufanya kupitia TEHAMA.
.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao(e-GA) Mhandisi Benedict Benny Ndomba amesema Kituo hicho kinafanya tafiti kwenye maeneo yote ya TEHAMA hasa kwenye Teknolojia zinazochipukia kama vile Bloc Chain, Artificial intelligence, Machine Learning, Cyber Security, Digital Currency nk.
.
Ndomba amesema kupitia Ubunifu, Utafiti na mazoezi kwenye maeneo hayo kama nchi tunakuwa kwenye nafasi nzuri ya kushindana kwenye uchumi wa kidijitali.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

