WAZIRI MKENDA AZINDUA MIONGOZO 4 YA ELIMU MAALUM NA JUMUISHI DODOMA
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof.Adolf Mkenda amesema lugha ya alama kwa walimu tarajali wanaopitia vyuo vya ualimu kuanzia hivi sasa itakuwa ni lazima kujifunza.
.
Mkenda ameyasema hayo Septemba 12,2023 alipokuwa akizindua Miongozo ya Elimu Maalum na Jumuishi Jijini Dodoma.
Amesema miongozo yote hiyo ni muhimu katika kutatua changamoto zinazoikabili wanafunzi wenye mahitaji maalum huku akisema matarajio ya Serikali katika miongozo hiyo ni kuleta chanya katika sekta ya Elimu hasa kwa kundi la watoto wenye mahitaji maalum.
.
Waziri Mkenda amesema,hatua hiyo ni kufuatia maono makubwa ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kutaka kutoachwa nyuma katika suala la Elimu kwa mtoto yeyote.
Aidha,Mkenda ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa kwa ViongozI na taasisi na wadau kuendelea kuhamasisha imuhimu wa Elimu maalum huku akiwahasa wazazi na walezi nchini wenye watoto hao waone umuhimu wa kuwaandikisha shule Ili Serikali ione jinsi ya kuwafikia hata wakiwa nyumbani.
.
Akitambulisha miongozo hiyo Mkurugenzi wa Elimu Maalum Dkt.Margareth Matonya ametaja miongozo hiyo kuwa ni Muongozo wa shule ya nyumbani kwa watoto ambao hawawezi kukaa darasani ambao amesema utawasaidia kuhakikisha watoto hao hawaachwi nyuma.
"Muongozo huu unalenga kuwafuata watoto majumbani na kuwafundisha masomo wanayofundishwa wengine shuleni."
Miongozo mingine ni wa ziara ya nyumbani ambao unaenda kuwasaidia upatikanaji wa taarifa wa akina nani wamefanyiwa ziara ya nyumbani na huu unawahusu hasa watoto wenye ulemavu wa usonji.
.
Kwa upande wake mzazi wa Mtoto Ally Kinara mwenye changamoto ya magonjwa adhimu aliishukuru Serikali kwa kuandaa na kuzindua Miongozo hiyo kwani watoto wengi walikiwa wanakosa haki muhimu ya kupata Elimu.
"Nakumbuka mwanangu Ally akiwa na miaka Saba aliona watu wakiwa wamevaa majoho na kofia,akaniuliza mama ili na Mimi nivae hivyo natakiwa nifanye Nini,pale ndio nikaona wakati muafaka wa Ally kwenda shule umefika.
"lakini nilipoenda kumuandikisha shule alikataliwa kutokana na Hali yake,nililia sana,lakini sikulia kwa ajili ya Ally,nililia huku jikijiuliza ni watoto wangapi hapa nchini wanakosa hii haki,kwa niishukiuru Serikali kwa kuleta miongozo hii ambayo sasa hata watoto wenye changamoto ya magonjwa adhimu sasa wanaenda kupata Elimu na kufikia ndoto zao" alisema Mzazi huyo.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

