logo

GEKUL AWASILISHA SHERIA NDOGO KWENYE KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul amewasilisha sheria ndogo ya kumlinda mtoa taarifa pamoja na mashahidi (The WhistleBlower and Witness Protection Act Cap. 446), katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo. Akiwasilisha mbele ya kamati Mhe.Gekul ameiambia kamati kuwa sheria hii ni muhimu na itasaidia katika kumlinda mtoa taarifa pamoja na ushaidi na kumpa mwongozo wa kudai haki zake mara tu baada ya ushaidi kukamilika.

Gekul amewasilisha Sheria hiyo leo tarehe 24, Agosti 2023 Kwenye ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma na kuwataka wajumbe watoe maoni pamoja mapendekezo ili kuweza kuboresha zaidi.

Kikao hicho ambacho kimeongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo Mhe. Ramadhan Suleiman Ramadhan (MB), ametoa mapendekezo ya kuwa katika sheria hii kuwepo na muundo mmoja wa uandishi wa barua ambao utatumika kujibu barua ya mwombaji wa ulinzi, ilikuepusha utofauti katika kujibu maombi hayo.

Vile vile kamati imependekeza kuwa muda wa Waziri kufanya maamuzi juu ya rufaa ya mwombaji wa ulinzi iwe ni siku 21 tu na si ndani ya siku 30 kama inavyoonyesha sasa. Hivyo kamati imetaka Waziri pamoja na watalaamu kufanya marekebisho katika vifungu hivyo.

Aidha, Kamati ipendekeza kuwa mwombaji apewe taarifa ya kukubaliwa au kukataliwa ombi la kulindwa kwa ndai ya siku 14 na iwapo mwombaji hataridhika basi anaweza kukata rufaa kwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Naibu Waziri Gekul ameishukuru Kamati kwa mapendekezo pamoja na maoni waliyotoa na kuahidi kufanyiwa kazi na kuleta sheria hiyo ambayo itakuwa imezingatia maboresho na maoni yote waliyopendekeza.

@katibanasheria_

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn