logo

TEA YAWATAKA WADAU WA ELIMU KUFANYA KAZI NA MFUKO WA ELIMU

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Ya Elimu Tanzania (TEA) Bi.Bahati Geuzye Ametoa Wito Kwa wachangajia Mbalimbali Wa Elimu waweze Kufanya Kazi Na Mfuko Wa Elimu Wa Taifa Ili kuwezesha Miradi Mbalimbali Nchini waliyoingia Makubaliano Nayo.

.

Geuzye Ameyasema Hayo Leo Agosti 10,2023 Alipokuwa akizungumza Na Waandishi Wa Habari Jijini Dodoma Kuhusu Utekelezaji Na Vipaumbele Vya TEA Kwa Mwaka 2023/24.

.

Amesema TEA Kupitia Mfuko Wa Elimu ilifadhili Miradi mikubwa Miwili Ikiwa Ni Pamoja Na Ujenzi Wa Shule Mpya Ya Msingi inayofundisha Kwa Lugha Ya Kiingereza Ya Msangalalee Kwa Thamani ya Shilingi Milioni 750 Katika Mwaka Wa Fedha Wa 2021/22.

.

"Mradi Huo umekamilika Katika Mwaka Wa Fedha 2022/23. Mfuko ulifadhili Ujenzi na Ukarabati Wa Miundombinu ya Elimu Katika Shule Nne za Msingi za Jijini Dodoma ambazo ni Kisasa,Kizota, Medeli Na Mlimwa 'C', Kwa Thamani Ya Sh.Bilioni 1.9 Mradi Huu ulianza Kutekelezwa Katika Mwaka Wa Fedha" Amesema Geuzye.

.

Mkurugenzi Huyo Amesema Kwa Mwaka 2022/23 Mamlaka hiyo ilipokea Michango na Kutekeleza Miradi ya Pamoja Na mashirika ya Umma na yasiyo ya Kiserikali Yenye thamani Ya Shilingi Milioni 404.

.

"Mashirika Hayo Yaliyoshirikiana na TEA ni Pamoja Na Shirika La Hifadhi za Taifa (TANAPA), BRAC Maendeleo Tanzania, Taasisi ya Asilimia Giving, Taasisi Ya Flaviana Matata, Taasisi Ya SAMAKIBA, CAMARA Education Tanzania Na Kampuni za Sayari Safi Na Dash Industries Ltd" Amesema Geuzye.

.

Aidha, Geuzye Amesema Kwa Mwaka Wa Fedha 2023/24, TEA imepanga Kutumia Kiasi Cha Shilingi Bilioni 8 Kwa Ajili Ya kufadhili Miradi ya Kuboresha Miundombinu ya Elimu Nchini.

.

"Kiasi Hicho kitatumika kufadhili Miradi 82 Katika Shule 81 zikiwemo Shule 48 za Msingi na 33 za Sekondari Katika Maeneo Mbalimbali ya Tanzania Bara".

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn