MPANJU: VYUO VIKUU WEKEZENI KATIKA ENEO LA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WATOTO
Wito Umetolewa Kwa Vyuo Vikuu Nchini Pamoja Na Ngazi Ya Elimu Ya Juu Kuwekeza Katika Eneo la Kutokomeza Ukatili Dhidi Ya Watoto kwa Kuangalia Namna Gani wanakuja na Mitaala mahususi kwenye Eneo la Malezi Ya Watoto Na Familia Ili kuweza Kusaidia Kupunguza Ukatili wa Watoto Katika Jamii.
.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wakili Amon Mpanju Leo Julai 13,2023 Alipokuwa Akifungua Mkutano Wa Taifa Wa Wadau Wa Malezi Na Kutokomeza Ukatili Dhidi Ya Watoto Katika Ukumbi Wa Rafiki Hotel Jijini Dodoma.
.
Amesema Chanzo Kikubwa Cha Ukatili Kwa Watoto na Suala Mmomonyoko Wa Maadili Kwa Jamii Sababu ni Ukosefu Wa Elimu Sahihi Ya Malezi na Makuzi ya Mtoto Kwa Watanzania.
"Kuna Kufeli Kwa Kushindwa Kufanya Kazi Kwa Mifumo ya Ustawi Wa Jamii, Kuna Migogoro Ndani ya Familia... Migogoro Ina Athiri Kizazi Cha Sasa Na Kijacho, Migogoro Katika Mwanamke na Mwanaume Madhara Yake ni Kupata Watu Ambao wamelelewa isivyo stahili" Amesema Mpanju.
.
Naibu Katibu Mkuu Huyo Amesema ni kweli Tunahitaji Kuongeza Juhudi ya kumlinda Mtoto Wa kike Lakini Kwa Hivi Sasa Muelekeo Wa Serikali ni Ulinzi Wa Mtoto Kwa Sababu Kila Mtoto Sasa Hivi ni muhanga Wa Ukatili.
.
"Watoto Wa Kiume wanalawitiwa, tunaanza Kuzalisha mashoga, Lakini uharibifu Unaanza Kutoka Chini wanaenda wanazoeshwa. Haya Yote Yanahitaji Tuje Na Mkakati ya kuyakabili kwa kuimarisha Malezi" Amesema Mpanju.
.
Mpanju Amesema Kwa Mujibu Wa Taarifa ya Tafiti iliyofanywa na Serikali na Shirika la UNICEF ilionyesha Asilimia Kubwa ya Vitendo vya Ukatili vinafanyikia Majumbani na Wazazi, Ndugu Jamaa Au Marafiki Ambao wanaoizunguka Familia.
.
Aidha, Mpanju Amesema lazima Kama Taifa Tuje na Mikakati Ya Kutokomeza Ukatili Huo kwa kueneza Elimu Kwa Jamii Kwani Tusipowekeza Katika Hilo na kuwasimamia Watoto na kuwaelimisha mapema, Sayansi itamkuta kitandani.
.
Naye Mkurugenzi Wa Idara Ya Maendeleo ya Mtoto Bw.Sebastian Kitiku Amesema Changamoto Kubwa waliyonayo Wazazi Katika Malezi inatokana na Maendeleo ya Teknolojia ya Habari Na Mawasiliano ambayo inawapelekea Wazazi washindwe kuwalea Watoto Vizuri.
.
Amesema Kutokana Na Hilo wao kama Serikali Wameamua kuja Na Muongozo Ambao utawaongoza Wadau( Ambao unaitwa Muongozo Wa Taifa Wa Wajibu Wa Wazazi na walezi Katika Malezi Ya Watoto na Familia).
.
Aidha, Kitiku Amesema Lengo la Mkutano Huo wao kama Serikali na Wadau Husika Kujenga Mazingira wezeshi Hasa Ya kisera Ili Kuongeza na kupanua wigo Wa Utekelezaji Wa Afua Za Malezi unaozingatia Ushahidi Wa Kisayansi.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

