JKT YATOA MSAADA MAKAO YA TAIFA YA KULELEA WATOTO KIKOMBO DODOMA
Katika Kuelekea Maadhimisho Ya Miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Jeshi Hilo Limeendelea Kutoa Msaada Kwa Jamii ikiwa Ni Sehemu ya Mchango wao Kwa Kujali Jamii ya watanzania ambapo Jana Julai 05,2023 Katika Kituo Cha Makao Ya Taifa Ya Kulelea Watoto Kikombo Jijini Dodoma,Limetoa Msaada wa chakula na Vitu Mbalimbali kwa ajili ya watoto wanaolelewa kituoni hapo.
.
Vitu vilivyotolewa ni pamoja na Kilogramu 500 za Mchele,Kilogramu 500 za Unga wa Sembe, Kilogramu 200 za Maharage,Kilogramu 50 za Sukari,Lita 60 za Mafuta Ya Alizeti, Juice Katoni 14, Chumvi Katoni 2, Pamoja Na Mbuzi wawili.
.
Akikabidhi Msaada Huo Kwa Niaba Ya Jeshi Hilo, Mkuu Wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena Amesema JKT limeona ni vyema watoto wanaolelewa katika Makao ya Taifa Kikombo wawe ni sehemu ya maadhimisho hayo.
.
Aidha amesema vitu vilivyopelekwa kituoni ni mafanikio ya JKT katika uzalishaji huku akisema,litakuwa likishirikiana Kila Wakati Wa Mavuno yao Kwa Mwaka kwa kupeleka chakula kituoni hapo kutokana na umuhimu wa lishe kwa watoto hao.
.
“Kwahiyo tutakuwa tunawasiliana na Uongozi Wa Kituo Hiki Ili Kuhakikisha Sehemu ya Mavuno yetu ya kila mwaka tunaleta hapa Makao ya Taifa ya Watoto Kikombo.
.
Ameongeza kuwa "Tutaendelea Kufanya Hivyo Hata Baadae Kuna Mazao Mengine Yanayotokana Na Ufugaji. JKT Tunafuga Nyuki, Siku Nyingine tutakuwa Tunakuja Na Asali iliyozalishwa Na Jeshi la Kujenga Taifa".
.
Amesema JKT Itaendelea Kushirikiana Na Kituo Hicho Katika Malezi Ya Vijana kuweza kuwapa Maarifa, Na Pia Jeshi Hilo litashirikiana Ili Kuhakikisha Kila Kitu kinakuwa Sawa.
.
Aidha, Brigedia Jenerali Mabena amewataka Walezi Wa Kituo Hicho kuwalea Na kuwatunza Watoto Hao Katika Kumfahamu Mungu Kupitia Dini Zao Na wafunzwe Kumjua Mungu Na Kusoma Kwa Bidii Na Pia waendelee Kufundishwa Kazi za Mikono.
.
Kwa Upande Wake Meneja Wa Kituo Hicho Bw.Tumaini John Ameliomba Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wanapokuwa Na Shughuli Nyingine zozote wasisahau Kituo Hicho Cha Kikombo Ili Watoto waweze Kuona Kwamba Jamii inawapenda Katika Mambo Mbalimbali.
.
Kituo Hicho Kilizinduliwa Tarehe 16 Mwezi Juni 2021 Na Makamu Wa Rais Dkt. Philip Mpango, na Kimeendelea Kupokea Watoto na kuwalea ambapo mpaka Sasa hivi Kina Jumla Ya Watoto 131.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

