WIKI YA UBUNIFU TANZANIA 2023 KUANZA APRIL 24-28
WAZIRI wa Elimu, Sayansi Na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Amesema Maadhimisho Ya Wiki Ya Ubunifu Tanzania 2023 yanatarajia Kufanyika Kabla Ya Shughuli za Kilele Tarehe 24 Mwezi April 2023 Katika Mikoa Tofauti Hapa Nchini.
.
Mkenda Ameyasema hayo Leo April 20,2023 Jijini Dodoma Alipokuwa Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Juu ya Maandalizi Kuelekea Wiki Ya Ubunifu Tanzania ambapo Kilele Chake Ni April 28,2023.
.
Waziri Huyo Amesema wiki Ya Ubunifu Inafanyika Kwa Ajili Ya Kutoa Fursa Kwa Wabunifu, Wagunduzi, watafiti, watunga Sera, Wadau Wa Maendeleo Na Washirika Wengine Kukutana Na Kujadili Sera, Kanuni Na Miongozo Mbalimbali Kuhusu Maendeleo ya Sayansi, Teknolojia Na Ubunifu.
.
"Kwa Mara ya Kwanza Safari Hii tutakuwa na Ushiriki kutoka Nchini Afrika Kusini, wiki Hii Muhimu inaanza Kuchukua Sura Ya Kimataifa" Amesema Mkenda.
.
Mkenda Amesema Maadhimisho Hayo Lengo Lake Ni kuimarisha Mfumo Wa Ubunifu hapa Nchini ambapo Juhudi hizo zimesaidia Wizara Husika Kuwa Na Bunifu Mbalimbali ambazo tayari zimeanza kuingia Sokoni.
.
"Hapa Nina Orodha Ya Bunifu 38 Mojawapo Ni Maarufu Sana ni Kwa Ajili Ya Mita Ya Maji ambayo inafanyiwa majaribio Sasa Hivi imeanza Kubiasharishwa" Amesema Waziri Huyo.
.
Aidha, Mkenda Amesema Mikoa 17 itakayofanyika Maadhimisho Hayo Ni Dodoma, Dar es Salaam, Morogoro,Mbeya,Iringa, Tanga, Arusha, Mwanza, Kigoma, Kagera, Mara, Njombe, Mtwara, Kilimanjaro, Songwe Na Unguja Magharibi Kupitia Kumbi Mbalimbali za Ubunifu.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

