MBUNGE MUSUKUMA AWATAKA WATANZANIA KUENDELEA KUUNGA MKONO AZIMIO LA SERIKALI
MBUNGE wa Geita Vijijini Mhe.Joseph Kasheku ‘Musukuma’ Amewaomba Watanzania wote Kuendelea Kuunga Mkono Azimio la Serikali Ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Kuingia Mkataba Na Serikali Ya Dubai Katika Ushirikiano Wa Kiuchumi na Kijamii Kwa Ajili Ya Uendelezaji Na Uboreshaji Na Utendaji Kazi Wa Bandari Tanzania Na Kama Kuna Mapungufu yakasimame kwenye Mkataba Wenyewe Husika.
.
Musukuma Ameyasema Hayo Leo Juni 9,2023 nyumbani Kwake Jijini Dodoma Wakati akizungumza Na Waandishi Wa Habari Juu ya Taarifa zilizosambaa Mtandaoni zikisema "Serikali imepanga kuipa Kampuni Ya DP World ya Falme za Dubai Kandarasi ya Uendeshaji Wa Shughuli za Bandari ya Dar es Salaam Kwa muda Wa Miaka 100".
.
Amesema Yeye anaamini Maneno yanayoandikwa kwenye Mitandao Sio ya Kweli, Kwa Sababu hata Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan atastaafu Na Ataishi Maisha kama Ya Watanzania wengine Na Sio Sahihi Kwamba atafunga Mkataba Hauna Maslahi Katika Taifa Hili.
.
"Tusikatishane Tamaa, Turudi Nyuma Watanzania, Hakuna Mradi Ambao Wa Kimkakati tumeufanya kwenye Awamu zote Bila Kuwa Na Kelele. Na Kelele Hizi zinatengenezwa Na Watu wasiotakia Maendeleo Nchi Yetu.
.
"Nakumbuka Mimi nilikuwa Kwenye Kamati ya Nishati na Madini Wakati Wa Uanzishwaji Wa Bwawa La Mwl.Nyerere kulikuwa na Mbwela Nyingi Sana Kuliko hata Hizi hapa. Lakini RAIS wa Awamu ya Tano Akasema tutajenga Bwawa, Leo imekuwa Siasa Kila Mtu anaombea Kura majimboni" Amesema Musukuma.
.
Mbunge Huyo Amesema Bandari ni Lango Kuu la Uchumi Na itakapo boreshwa Watanzania wasubiri kuja Kuulizana na anaamini wanaopiga Kelele ni Chuki Tu walizonazo.
.
""Kama tuna Lengo zuri la Kuisaidia Nchi Yetu Huu ndio Wakati muafaka Wa Kutoka hatua tuliyokuwa nayo Kwenda kwenye Hatua Nyingine" Amesema Musukuma.
Aidha, Musukuma Ameishauri Serikali kuchukua Waandishi Wa Habari Wa Kutosha Ili iwapeleke Nchini Dubai wakaone Bandari Yao ilivyoendelea.
.
"Uchumi Wa Watanzania haumilikiwi na Watu Wenye Degree Hawa wanaoutusumbua mitandaoni, Uchumi Wa Watanzania unamilikiwa Na Sisi Wenyewe Ya Kawaida" Amesema Musukuma.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news