logo

MWENGE WARIDHISHWA NA UJENZI WA OFISI NA MAABARA ZA TAEC ZANZIBAR

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2023 Ndugu Abdallah Shaib Kaim ameridhishwa na ujenzi wa ofisi na maabara za Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania upande wa Zanzibar zinazojengwa eneo la Dunga Zuze.

Ndugu Abdallah ameyasema hayo baada ya Mwenge wa Uhuru kutembelea mradi huo utakaokuwa na ofisi 27 na maabara sita.

.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania Prof. Lazaro Busagala ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Rais Dkt. Hussein Mwinyi kwa namna wanavyosaidia mradi huo kufanikiwa ambapo utakuwa na manufaa ya kiuchumi kijamii na usalama kwa nchi.

.

Mradi wa ujenzi wa Ofisi na Maabara za Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Zanzibar umefikia asilimia 85 na mkandarasi ameshalipwa 59% ya malipo ya mradi.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn