DCEA YAFICHUA MIRUNGI, SKANKA KUSAFIRISHWA KWENYE MAGARI YA MAITI
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema baadhi ya magari yanayosafirisha maiti kwenda mikoa mbalimbali nchini yameanza kutumiwa na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kusafirisha mirungi, bangi na skanka.
.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas James Lyimo, amesema hayo leo Jumanne, Septemba 29, 2026, jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu operesheni za kudhibiti dawa za kulevya zilizofanyika katika mikoa 14 kati ya Julai na Septemba mwaka huu.
.
Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Mara, Dodoma, Mbeya, Lindi, Mtwara na Ruvuma.
.
Kwa mujibu wa Lyimo, taarifa za kiintelijensia zimebaini kuwa baadhi ya magari yanayosafirisha maiti kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya Kaskazini, ikiwemo Kilimanjaro, Arusha na Tanga, yamekuwa yakitumiwa kusafirisha dawa za kulevya wakati yanaporejea kutoka kwenye misiba.
.
Amesema baadhi ya magari yanayoelekea Kaskazini yamekuwa yakibeba skanka, huku mengine yanaporejea Dar es Salaam yakibeba mirungi.
.
Lyimo pia amesema baadhi ya dawa hizo zimekuwa zikipelekwa katika maeneo yanakofanyika misiba, akieleza kuwa mirungi ni miongoni mwa dawa zinazotumiwa katika mazingira hayo.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

