logo

TUMIENI MUDA VIZURI MNAPOPATA NAFASI YA KWENDA  JKT- MHE.PINDA

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda, amewataka Vijana nchini kutumia muda vizuri wanapopata nafasi ya kwenda Jeshi la Kujenga Taifa ( JKT).

‎Mhe. Pinda ameyasema hayo Agosti 6,2026 wakati alipotembelea Banda la JKT katika Maonesho ya Wakulima (Nanenane), yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Malecela, Nzuguni Dodoma.

‎"Sisi tuliopita JKT miaka ya zamani huko, hatuna budi kuwaambia vijana wa leo kwamba tumieni muda huu vizuri mnapopata nafasi ya kwenda JKT, JKT ambayo sasa inalenga kuwaimarisha vijana na kuwapa uwezo wa kuweza kuanza maisha yao wenyewe kutokana na ujuzi walioupata kutoka maeneo ya makambi ya JKT"

‎Amefafanua kuwa JKT ni shule nzuri kwa vijana, kwani limetengeneza utaratibu mzuri wa kuwapa mafunzo vijana hususani katika suala zima la ubunifu. Vijana wanafundishwa ubunifu wa kutengeneza vitu mbalimbali vinaweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn