logo

DG NEMC AKITOA NENO LA UKARIBISHO WAKATI WA FUTARI HOTEL YA SERENA JIJINI DAR ES SALAAM

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeungana na wadau wa mazingira katika hafla ya futari iliyoandaliwa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kuendeleza mahusiano mazuri baina ya taasisi hiyo na wadau wake.

‎Hafla hiyo imefanyika Februari 26,2026 katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi, watumishi wa Serikali na wadau binafsi walihudhuria tukio hilo lenye taswira ya umoja na mshikamano.

‎Akizungumza katika hafla hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Hamza S. Johari ameipongeza NEMC kwa kuandaa tukio hilo lenye kujenga umoja na kukuza mshikamano miongoni mwa Taasisi za Serikali na wadau wa mazingira.

‎.

‎Aidha, ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa kisheria ili kuhakikisha Sheria na Kanuni za mazingira zinatekelezwa ipasavyo kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

‎Naye Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi, amesema futari hiyo ni sehemu ya utamaduni wa Baraza katika kujenga uhusiano wa karibu na wadau wake.

‎Amesisitiza umuhimu wa kudumisha maadili ya utu, heshima na ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya hifadhi ya mazingira nchini, akibainisha kuwa kupitia ushirikiano huo malengo ya kulinda na kuboresha mazingira yanaweza kufikiwa kwa ufanisi zaidi.

‎Katika hatua nyingine Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Abdul Rajabu Mhinte, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya NEMC na Ofisi ya Mkoa katika kusimamia na kutekeleza Sheria za mazingira.

‎.

‎Ameahidi kuwa Ofisi ya Mkoa itaendelea kuunga mkono juhudi za uhifadhi na usimamizi endelevu wa mazingira kwa ustawi wa taifa.

‎Hafla hiyo imehudhuriwa pia na wadau wa mazingira wakiwemo JMAT, Bodi ya NEMC, watumishi wa Baraza, wawakilishi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Taasisi za kibenki.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn