MADEREVA MALORI WATAKIWA KUPEWA ELIMU JUU YA MADHARA YA KEMIKALI
WITO umetolewa Kwa wamiliki wa Malori Nchini Kuhakikisha madereva wao wanapewa Elimu Kwa Ufasaha Ili waweze kwenda kujilinda na wasipate Madhara Wakati ambapo wanasafirisha Kemikali.
.
Msajili Wa Vyama Vya Wafanyakazi Na Waajiri Bi.Pendo Berege Ametoa Wito Huo Leo Mei 24 Jijini Dodoma Alipokuwa Akifungua Mafunzo Ya Madhara Ya Kemikali Kwa Viongozi Wa Vyama Vya Madereva Katika Ukumbi Wa Jengo la Mkemia Mkuu Wa Serikali.
.
Berege Amesema Kwa Mujibu Wa Sheria ya Kudhibiti Kemikali, Mwenye Mamlaka ya Kutoa Mafunzo na Elimu Kuhusiana na Masuala ya Kemikali Ni ofisi Ya Mkemia Mkuu Tu na Sio Watu wengine Wala Chama Cha Wafanyakazi hivyo wanapaswa Kufuata Sheria Na Kanuni Husika.
.
"Kwahiyo Madereva kama Umekutana Na Changamoto yoyote Hatua Ya Kwanza ni Kuwafikia Wahusika Ambao Kwa Mujibu Wa Sheria ndio wamepewa hiyo Mamlaka ya Kufanya Utaratibu Huo na Kutoa Mafunzo Hayo.
.
"Kuwafikia, Kuwaeleza Na Kwa Pamoja wanakwenda Kutoa Mafunzo. Hii Siyo Kazi Ya Chama Cha Wafanyakazi, Tuungane Na Tufuate Sheria" Amesema Berege.
.
Msajili Huyo Amesema Lengo la Mafunzo Hayo Ni Madereva waweze Kupata Uelewa Juu ya Usafirishaji Wa Kemikali Kutoka Sehemu Moja Kwenda Sehemu Nyingine Ili kuweza kulinda Mazingira Yetu na Kuendelea Kupata Pato la Uchumi Wa Nchi.
.
Aidha, Berege Amesema matarajio yake Baada ya Mafunzo Hayo Madereva wataweza Kuzingatia taratibu za Kisheria za utoaji Wa Taarifa zinazohusiana na Masuala ya Sumu na Kemikali na Pia Watazingatia Usafirishaji Salama Wa Kemikali.
.
Nae Mwenyekiti Wa Chama Cha Madereva Tanzania (TADWU) Bw. Schubert G. Mbakizao Amesema wao kama Viongozi Wa Madereva Kazi Yao Ni Kuhakikisha Kwamba wanalinda Vyanzo Ambavyo vinaweza Kusapoti Serikali iweze Kuviendeleza Hususani kwenye Bandari Zetu.
.
Mbakizao Ameiomba Serikali Kutumia Nguvu Kubwa Ya Kulinda Sekta Ya uchukuzi Ili iendelee kuajiri Madereva.
.
"Sasa Hivi Mizinga Mizinga Imepungua Kwa Sababu Kila Mtu yupo Kazini, ikiwa tutaleta Shida Kidogo au Tutaacha Watu wanaotaka Kuleta Shida" Amesema Mbakizao.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

