logo

WACHEZAJI WAZAWA KUING'ARISHA JKT QUEENS KIMATAIFA NCHINI MISRI

MKUU wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele amewataka watanzania kuiunga mkono timu ya JKT Queens inayokwenda kuliwakilisha Taifa na ukanda wa CECAFA katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa upande wa soka la wanawake.

‎Meja Jenerali Mabele ameyasema hayo mara baada kumalizika kwa zoezi la upangaji wa makundi lililofanyika Cairo nchini Misri Oktoba 27,2025 ambapo JKT Queens imepangwa Kundi B likijumuisha Bingwa mtetezi TP Mazembe kutoka DR Congo, Asec Mimosas kutoka Ivory Coast na Gaborone United kutoka Botswana.

‎Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 08, 2025 hadi Novemba 21,2025.

‎Aidha, Meja Jenerali Mabele ametoa wito kwa watanzania kushabikia timu hiyo ya kizalendo yenye wachezaji wazawa kama inavyofanyika mara zote kwa kwa timu za Simba na Yanga zinapowakilisha nchi.

JKT Queens inawakilisha Tanzania na Ukanda wa CECAFA kwa ujumla kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa Wanawake ambapo jumla ya timu 8 zitashiriki.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn