logo

TAEC YABORESHA HUDUMA ZAKE JIJINI MWANZA

SERIKALI kupitia Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) inaendelea na ujenzi wa ofisi mpya pamoja na maabara katika Kata ya Mkolani Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza.

Mkuu wa Ofisi ya Kanda ya Ziwa, Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania Bw. Miguta Ngulimi amesema dhamira ya serikali ni kusogeza huduma karibu na wananchi na kukamilika kwa ujenzi huo kutasaidia huduma za vibali vya mionzi pamoja na ukaguzi wa watumiaji wa vyanzo vya mionzi.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania Bw.Peter Ngamilo amesema uboreshaji wa ofisi unaendelea maeneo mbalimbali nchini ili kusogeza huduma karibu na wananchi.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn