ABIRIA NA MIZIGO IMEONGEZEKA KWENYE NDEGE ZA ATCL -WAZIRI MBARAWA
“Mhe. Spika, Katika mwaka wa fedha 2024/25, Serikali imeendelea kufufua ATCL kwa kununua ndege, kuboresha karakana za matengenezo ya ndege, na kutekeleza mikakati ya kuongeza ubora na usalama katika utendaji ili kutoa huduma ya usafiri wa abiria na usafirishaji wa mizigo.
Mhe. Spika, Serikali katika Mwaka wa Fedha 2024/25 imekamilisha ununuzi wa ndege aina ya Boeing 787-8 Dreamliner na kufanya ATCL kuwa na jumla ya ndege 16. Uwepo wa ndege hizo umeiwezesha ATCL kupanua mtandao wa safari na kuifanya ATCL kuwa na vituo 27 vinavyotoa huduma. Kati ya vituo hivyo: vituo 15 ni vya ndani ya nchi, Vituo tisa (9) ni vya kikanda na Vituo vitatu (3) ni vya kimataifa.
Katika kipindi cha Julai, 2024 hadi Machi 2025, ATCL imesafirisha abiria 876,357 sawa na ongezeko la abiria 25,697 ikilinganishwa na abiria 850,660 waliosafirishwa katika kipindi kama hicho mwaka 2023/24. Pia, ATCL ilisafirisha tani 5,869.81 za mizigo sawa na ongezeko la tani 835.61 ikilinganishwa na tani 5,034.2 zilizosafirishwa katika kipindi kama hicho mwaka 2023/24.” -Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi akiwasilisha bajeti ya Wizara ya uchukuzi kwa mwaka 2025/26.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

