logo

UCSAF YAPANGA KUFIKISHA VIFAA VYA TEHAMA SHULE 22 ZA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM NCHINI

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi Peter Mwasalyanda, amesema wamepanga kufikisha vifaa vya TEHAMA katika Shule 22 nchini ambazo zina watoto wenye mahitaji maalum.

.

"Vifaa vya TEHAMA hivyo ni pamoja na TV, Braille Machine (Nukta Nundu) Orbit reader (Machine za Kisasa), Laptops, Embosser (Printa ya nukta nundu), Digital voice recorders, Magnifiers" alisema.

.

Mha. Mwasalyanda ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mfuko huo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo Machi 27, 2025,Jijini Dodoma.

.

Amesema katika kipindi cha miaka minne ya Awamu ya sita, shule takribani 469 zimepelekewa vifaa vya TEHAMA huku lengo ni kukuza ujuzi wa TEHAMA kwa Wanafunzi na Walimu nchini.

.

Mha. Mwasalyanda amesema hadi kufikia tarehe 24 mwezi Machi,2025 minara 430 imejengwa na kuanza kutoa huduma kwa wananchi wa maeneo ya vijijini.

.

Aidha, amesema Serikali inatambua umuhimu wa shirika la Posta nchini na hivyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita, Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote imekuwa ikiliwezesha shirika la Posta kwa kulipatia vifaa vya TEHAMA ili shirika liweze kutoa huduma kidigitali.

.

"Tarehe 12 Julai 2024, UCSAF ilinunua PDA 250 na kuwakabidhi Shirika la Posta, Gharama za utekelezaji wa mradi huu ni kiasi cha TZS 161,926,471/=, Mwezi Aprili 2025, UCSAF itakabidhi vifaa vingine 250 kwa shirika la Posta vyenye thamani ya TZS 161,926,471/=" alisema.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn