logo

PAPA FRANCISCO AMTEUA ASKOFU MUSOMBA KUWA ASKOFU WA KWANZA JIMBO KATOLIKI BAGAMOYO

Baba Mtakatifu Fransisko amemteua Askofu Stephano Lameck Musomba, O.S.A, kuwa Askofu wa Kwanza Jimbo Katoliki Bagamoyo.

Askofu Musomba ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam na baada ya uteuzi huu atakuwa Askofu wa Jimbo jipya Katoliki Bagamoyo ambalo limeanzishwa leo Machi 7, 2025.

Mhashamu Askofu Musomba alizaliwa Septemba 25,1969 Malonji Jimbo Kuu Katoliki Mbeya.

Baada ya masomo yake ya upadre, alipewa Daraja Takatifu la upadre Julai 24, 2003 na kuhudumu katika nafasi mbalimbali za utume shirikani, Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Morogoro.

Hadi uteuzi wake Mhashamu Askofu Musómba alikuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam tangu mwaka 2021.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn