logo

WAZIRI SILAA AFUNGUA MAADHIMISHO YA WIKI YA ANWANI ZA MAKAZI NCHINI JIJINI DODOMA

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Jerry Silaa, ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanazifahamu anwani zao za makazi na kuzitumia katika kujitambulisha; kwa ufafanuzi zaidi wafike kwa watendaji wa Mitaa, Vijiji ama Shehia au kwa Waratibu wa Mfumo wa Anwani za Makazi wa Halmashauri.

.

Silaa ameyasema hayo leo February 06,2025 alipokuwa kwenye Maadhimisho ya Wiki Ya Anwani za Makazi Nchini katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Conversion Center Jijini Dodoma.

.

Amesema Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa kila nyumba, jengo, kiwanja, huduma, ofisi ama eneo la biashara linatambulika kwa Anwani ya Makazi.

.

"Anwani ya Makazi inaundwa na Namba ya Anwani maarufu kama namba ya nyumba; Jina la Barabara au Mtaa; na Postikodi. Postikodi ama nchi zingine zinaita Zipcode ni utaalamu wa kugawa maeneo ili kurahisisha utambuzi" alisema Silaa.

.

Waziri Silaa amesema mfumo wa Anwani za Makazi unarahisisha utoaji na upokeaji wa huduma mbalimbali ili kuchochea maendeleo ya Kiuchumi na kijamii hasa katika zama hizi ambazo Mapinduzi ya 4,5 na 6 ya viwanda yanategemea matumizi ya TEHAMA.

.

Aidha, Silaa amesema Utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi ni endelevu kwa sababu ya mabadiliko ya makazi, wakazi, na huduma.

.

"Hivyo, shughuli mbalimbali za Mfumo zinaendelea kutekelezwa ikiwemo kukusanya, kuhakiki na kuhuisha taarifa za Anwani za Makazi; kuboresha utendaji kazi wa Mfumo wa NaPA; kutoa elimu kwa umma na kuhamasisha utekelezaji, uendelezaji na matumizi ya Mfumo wa Anwani za Makazi" alisema Silaa.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn