ELIMU YA URAIA NA UTAWALA BORA IWAFIKIE WANANCHI ILI WATAMBUE HAKI ZAO -RAS IGUNGA ELIZABETH
Katibu Tawala wa Wilaya ya Igunga Bi. Elizabeth Emmanuel amewataka Washiriki wa mafunzo ya elimu ya uraia na utawala bora kuisambaza elimu hiyo waliyopewa kwa wananchi wao ili kila mtanzania atambue haki zake kwa mujibu wa sheria
Bi.Elizabeth ametoa wito huyo wakati akifungua mafunzo ya hayo yananyoendeshwa na Wizara ya Katiba na Sheria kwa kamati ya usalama wilaya ya igunga ,watendaji wa kata na baadhi ya watumishi wa wilaya hiyo
Aidha, Bi.Elizabeth ameishukuru Wizara ya Katiba na Sheria kwa kuwaletea Mafunzo hayo kwani yatakuwa chachu ya kuleta mabadiliko miongoni mwao katika usimamizi katika usimamizi na ulinzi wa haki za binadamu na misingi ya utawala Bora.
Kwa upande wake Wakili wa Serikali Kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi.Dorice Dario amesema malengo ya kutoa elimu hiyo ni kuwajengea uwezo Viongozi wa Malmlaka za Serikali za Mitaa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Kuwanongezea ufanisi katika utendaji kazi. Pia aliwasihi kufanya kazi kwa kuzingatia utu wa kila mwananchi wanaemhudumia.
Akiwasilisha mada kuhusu madaraka kwa umma mbele ya washiriki Mashaka Makuka amesema wananchi wanapaswa kupewa mrejesho wa changamoto zao mapema ili iwape Imani na serikali yao.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

