logo

SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO YA MWAKA 2015, JAMII MUIJUE -JONGO

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Bw. Ramadhani Jongo kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, ametoa wito kwa jamii kuisoma na kuijua Sheria ya ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 ambayo inapatikana katika tovuti ya Wizara hiyo (www.mawasiliano.go.tz) na tovuti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (www.tcra.go.tz) kwa lengo la kufahamu haki na wajibu wao katika sheria hiyo.

Wito huo umetolewa Novemba 22, 2024 katika ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma alipokuwa akizungumzia masuala ya matumizi salama ya mtandao.

Ameongeza kuwa, sheria hiyo inaelezea bayana makosa ya mtandao ni yapi na adhabu zake ni zipi hivyo jamii inapaswa kuifahamu vizuri sheria hiyo ili kuwa na uelewa mpana wa haki zao na wajibu wao, kwani kutokujua sheria hakumuondolei mtu hatia pale anapovunja sheria.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn